Jifunze ambacho Tor Browser inaweza kufanya kwa kulinda faragha zako na kutojulikana
Jinsi ya kupakua Tor Browser
Kusanikisha Tor Browser kwa ajili ya kutumia
Jifunze jinsi ya kutumia Kivinjari Tor kwa mara ya kwanza
Ufanye nini kama mtandao wa Tor umezuiliwa
Pluggable Transports nyingi, kama vileobfs4, hutegemea matumizi ya "bridge" relays
Jifunze namna ya kudhibiti taarifa za utambulisho binafsi katika Tor Browser
Huduma ambazo zinapatikana tu kwa kutumia Tor
Jifunze jinsi ya kulinda data yako kwa kutumia Tor Kivinjari and HTTPS
Kusanidi Tor Browser kwa ajili ya usalama na matumizi
Jinsi ya kusasisha Tor Kivinjari
Nini cha kufanya kama Tor Browser haifanyi kazi
Kwa namna gani Tor Browser huzibiti vitu vya nyongeza, programu jalizi na JavaScript
Namna ya kutoa Tor Browser katika mfumo wako
Maswala yanayojulikana
Jifunze kuhusiana na huduma za Tor kwa vifaa vya mkononi
Jinsi ya kufungua Tor Kivinjari kwenye media inayoweza kutolewa
Namna ya kupata msaada,toa taarifa ya tatizo au toa mrejesho
Tor Browser hutumia mtandao wa Tor kulinda faragha yako na kutojulikana. kutumia mtandao wa Tor kuna sifa kuu mbili:
Mtoa huduma wa mtandao wako, na yeyote anayeangalia mawasiliano yako ya ndani, hatoweza kufuatilia shughuli zako kwenye mtandao, ikijumuisha majina na anwani za tovuti unazotembelea.
waendeshaji wa tovuti na huduma unazotumia, na yeyote anayewaangalia,ataona mawasiliano yanatoka mtandao wa Tor badala ya anwani ya mtandao wako halisi, na hatajua wewe ni nani mpaka utakapojitambulisha.
Kwa kuongezea, Tor Browser imetengenezwa kuzuia tovuti kufanya “fingerprinting”au kukutambua kulingana na uundwaji wa kivinjari chako.
Moja kwa moja Tor Browser haitunzi kumbukumbu yoyote ya kuperuzi. Vidakuzi hufanya kazi kwa kipindi kimoja tu (mpaka Tor Browser inapotolewa au New identity inapoombwa).
Tor ni mtandao usioonekana kwa kushikika uliofichwa unaokuruhusu kuboresha faragha yako na usalama katika mtandao. Tor hufanya kazi kwa kusafirisha taarifa zako katika seva tatu zisizo katika mpangilio (pia hufahamika kama relays) katika mtandao wa Tor. Relay ya mwisho katika circuit (“exit relay") kisha hutuma taarifa katika mtandao wa umma.
Picha hapo juu inaonyesha mtumiaji wa kivinjari katika tovuti mbalimbali badala ya Tor. Kompyuta ya kijani ya katikati inawakilisha relays kwenye mtandao wa Tor, wakati funguo tatu zinawakilisha matabaka ya usimbaji wa kila relay.
Njia salama na rahisi ya kupakua Tor Browser ni kutoka katika tovuti rasmi ya Tor Project katika https://www.torproject.org/download. Mawasiliano yako katika tovuti yatakuwa salama kwa kutumia HTTPS,ambayo huleta ugumu zaidi kwa mtu kucheza nayo.
Hatahivyo, kuna wakati ambapo huwezi kuipata tocuti ya Tor Project kwa mfano, kama itakuwa imezuiliwa katika mtandao wako. Kama hii ikitokea, unaweza kutumia moja ya njia za kupakua zifuatazo za mbadala:
Kama unashindwa kupakua Tor Browser kutoka katika tovuti rasmi ya Tor Project, badala yake unaweza kuipakua kutoka katika moja ya nakala zetu rasmi, inaweza kuwa kwa kupitia EFF or Calyx Institute.
GetTor ni huduma ambayo mojakwamoja hujibu ujumbe wenye anwani za toleo jipya la Tor Browser, lililopo sehemu mbalimbali, kama vile Dropbox, Google Drive and GitHub.
Tuma barua pepe kwenda gettor@torproject.org,na katika ujumbe kwa ufupi andika “windows”, “osx”, au(((“linux”,(bila alama za funga na fungua semi) kufuatana na mfumo wako wa uchakataji. Kwa mfano ili kupata anwani za kupakua Tor Browser kwa ajili ya Windows, tuma barua pepe kwenda gettor@torproject.org l ikiwa na neno "windows" katika kichwa cha habari.
GetTor itaoa majibu yakiwa na barua pepe yenye anwani ambayo unaweza kupakua Tor Browser, saini ya kriptografia (inahitajika ili kuhakiki upakuliwaji), alama za kipekee za funguo hutumika kutengeneza saini, na vifurushi checksum. Unaweza kupewa chaguo la programu yenye ukubwa wa “32-bit” or “64-bit” kulingana na aina ya kumpyuta unayotumia.
Tuma ujumbe kwenda @GetTor_Bot kupitia Telegram.
Bofya 'Start' au write /start
katika mawasiliano.
Chagua lugha yako.
Kuna machaguo mawili ya kupakuaT or Browser.
1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.
Pakua faili la .exe
Windows .
(Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.
Upakuaji ukikamilika, bofya mara mbili kitufe cha faili la .exe
. Kamilisha zoezi la kuweka programu ili uweze kutumia.
1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.
Pakua faili la macOS .dmg
.
(Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.
Upakuaji ukikamilika, bofya mara mbili kitufe cha file la .dmg
. kamilisha zoezi la kuweka program ili uweze kutumia.
1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.
Pakua faili la GNU/Linux .tar.xz
.
(Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.
Sasa fuata njia ya picha au ya amri za maelezo:
Ukimaliza kupakua, chuja mafaili yaliyohifadhuwa.
utaitaji kuiambia GNU/Linux kuwa unahitaji uwezo wa kumia maneno yenye amri .
Peruzi katika saraka ya Tor Browser.
Bofya kulia katika start-tor-browser.desktop
, fungua Properties au Preferences na badilisha ruhusa ya kuruhusu faili lenye maandishi ya amri kuwa kama programu.
Bofya mara mbili kitufe cha Tor Browser ili kuanza kutumia kwa mara ya kwanza.
Zingatia Katika Obuntu na baadhi ya vyanzo vingine vya wazi kama ukijaribu kufungua start-tor-browser.desktop
faili lenye maneno linaweza kufunguka.
In that case, you will have to change the default behavior and allow running .desktop files as executables.
This setting can usually be found in your file manager.
ukimaliza kupakua chuja mafaili yaliyohifadhiwa kwa amri tar -xf [TB archive]
.
Kutoka ndani ya saraka ya Tor Browser, unaweza kufungua Tor Browser:
./start-tor-browser.desktop
Zingatiakama amri hizi zitashindwa kufanya kazi, pengine utahitajika kutengeneza faili lenye amri. Ambayo inataokana na utendaji wa saraka chmod +x start-tor-browser.desktop
Baadhi ya ishara zinazoweka kutumika na start-tor-browser.desktop
kutoka katika orodha ya maelezo ya amri:
Flag | Maelekezo |
---|---|
--register-app |
Kusajili Tor Browser kama program ya kompyuta. |
--verbose |
Kuonyesha matokeo ya Tor na Firefox katika kifaa unachotumia. |
--log [file] |
Kuchukua taarifa za matokeo ya Tor na Firefox katika faili (default: tor-browser.log). |
--detach |
Kutoka katika muunganiko na kutumia Tor Browser pembeni. |
--unregister-app |
Kuondoa usajili wa Tor Browser kama programnu ya komyuta. |
Angalia hapa namna ya kuhuwisha Tor Browser.
Unapoanza Tor Browser, utaona windo inayokuambia jiunge na Tor. Hii inakupelekea wewe chaguo kuunganisha moja kwa moja kwenye mtandao wa Tor, au kupangilia Tor Kivinjari kwenye muunganisho wako. Kuna uhakiki ambao utakuuliza kama unahitaji kujiunga mojakwamoja katika mtandao wa Tor, kama ndivyo, angalia.
Mara nyingi, kuchagua"Connect" itakuruhusu kuunganisha katika mtandao wa Tor bila usanidi wa ziada.
Utakapobofya, mstari wa hali utatokear, kuonyesha mawasiliano ya Tor yanayoendelea. Kama upo katika mtandao wenye kasi, lakini sehemu hiyo inakwama katika eneo fulani, jaribu 'Connection Assist' au angaliaTroubleshooting kurasa ya msaadan kwa ajili ya kutatua matatizo. Or, if you know that your connection is censored or uses a proxy, you should click on "Configure Connection".
Kama Tor imezuiliwa katika eneo lako, jaribu bridge inaweza saidia. Connection Assist inaweza kuchagua moja kwa ajili yako kutumia eneo.
Kama Connection Assist haiwezi kutambua eneo lako au unataka kusanidi mawasiliano yako wewe mwenyewe badala ya,unaweza kuchagua eneo ulilopo kutoka katika menyu iliyo na orodha kisha bofya katika 'Try a Bridge'.
Tor Browser itakupeleka katika machaguo kadhaa ya kusanidi.
Connection Assist iitakutaarifu kuhusiana na hali ya mawasiliano yako ua mtandao na mawasiliano yako katika mtandao wa Tor.
Orodha ya kwanza ya kuhakiki ni 'Quickstart'. Kama imechaguliwa, kila mara unapoifungua Tor Browser, itajaribu kuunganishwa na mipangilio ya mtandao iliyopita.
Kama unajua kuwa mtandao wako umedhibitiwa, au umejaribu na umeshundwa kujiunga na mtandao wa Tor na hakuna suluhusho lingine lililofanikiwa, unaweza kusanidi Tor Browser kwa kutumia usafirishaji wa pluggable . 'Bridges'zitaonyesha Ukwepaji wa udhibiti wa mtandao sehemu ya kusanidi usafirishaji wa pluggable au kuunganisha kwa kutumia Bridges.
Kama mawasiliano yako yanatumia proxy unaweza kusanidi kwa kubofya 'Settings ...' against 'Sanidi namna Tor Browser huunganishwa katika mtandao'. Katika matukio mengi, hii siyo lazima. Kwa kawaida utajua kama unahitaji kuchagua uhakiki huo sababu mpangilio huohuo utatumika kwa kivinjari kingine katika mfumo wako. Kama inawezakana, mulize msimamizi wako wa mtandao kwa muongozo. Kama mawasiliano yako hayatumii proxy, bofya"Connect".
Upatikanaji wa mojakwamoja wa mtandao wa Tor wakati mwingine unaweza kuzuiliwa na mtoa huduma wako wa mtandao au serikali. Tor Browser inajumuisha baadhi ya vifaa vya kukwepa uzuiliwaji wa mtandao kwa kuweza kuwepa uzuiliwaji huo. Vifaa hivi vinaitwa “pluggable transports”.
Currently there are four pluggable transports available, but more are being developed.
obfs4 | obfs4 hufanya usafirishaji wa Tor kuwa hauna mpangilio, na pia huzuia wazibiti kupata bridges kwa kuchunguza mtandao, obfs4 bridges zinauwezekano mdogo sana kuzuiliwa kuliko vitangulizi, obfs3 bridges. |
meek | Usafirishaji wa meek huwa kama unaperuzi tovuti kubwa badala ya kutumia Tor, meek-azur hufanya kuwa kama unatumia tovuti ya Microsoft. |
Snowflake | Snowflake routes your connection through volunteer-operated proxies to make it look like you're placing a video call instead of using Tor. |
WebTunnel | WebTunnel masks your Tor connection, making it appear as if you're accessing a website via HTTPS. |
Kutumia pluggable transport, bofya "Configure Connection" unapoanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika menu, chagua pluggable transport ambayo ungependa kuitumia.
Pale unapokuwa umechagua pluggable transport, pandisha juu na bofya "Connect" kuhifadhi mpangilio.
Au, kama Tor Browser inatumika, bofya "Settings" katika machaguo (≡)na kisha katika "Connection" katika mstari wa pembeni. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Chagua pluggable transport yoyote unayopenda kutumia toka katika orodha ya machaguo. Mpangilio wako kiautomatiki utahifadhiwa mara utapofunga tabo.
Kila moja katika usafirishaji ulio orodheshwa katika munu ya Tor Bridge huwafanya kazi katika njia tofauti, na ufanisi wake hutegemea mazingina ya mtu binafsi.
Kama unajaribu kukwepa uzuiliwaji wa mawasiliano kwa mara ya kwanza, unatakiwa kujaribu namna nyingine ya usafirishaji :obfs4, snowflake au meek-azure.
Kama unajaribu njia zote hizo, na hakuna inayokuwezesha kupata mtandao, utahitajika kuomba bridge au ingiza anwani ya bridge kawaida.
Watumiaji nchini China watatakiwa kujiunga na obfs4 bridge binafsi ambazo hazijaorodheshwa.
Wasiliana nasi kupita Telegram Bot @GetBridgesBot and type /bridges
.
Au tuma barua pepe kwendafrontdesk@torproject.org ikiwa na maneno "private bridge cn" katika kichwa cha habari.
If you're connecting from other country, please remember to include your country or country code in the subject of the email.
Soma sehemu ya Bridgeskujua bridge ni nini na namna ya kuzipata.
Pluggable Transports nyingi, kama vile obfs4, zinategemea matumizi ya "bridge" relays. Kama ilivyo Tor relays za kawaida, madaraja yanaendeshwa na wanaojitolea; tofauti na relays za kawaida,zenyewe hazijaorodheshwa wazi, ili mtu asiye na nia njema akazitambua kwa urahisi.
Kutumia Bridges pamoja na pluggable transports husaidia kuondoa ukweli kwamba unatumia Tor, ila inaweza kupunguza kasi ya mawasiliano ukilinganisha na unapotumia Tor relays za kawaida.
Other pluggable transports, like meek and Snowflake, use different anti-censorship techniques that do not rely on finding bridge addresses. You do not need to obtain bridge addresses in order to use these transports.
Kwasababu anwani za bridge sio za umma, unatatakiwa kuomba wewe mwenyewe. una machaguzi machache:
/start
or/bridges
katika mawasiliano ya ujumbe. Nakili anwani ya bridge na endelea:Kama unaanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza, bofya katika "sanidi muungamisho"kufungua ukurasa wa mpangilio wa Tor. Chini ya eneo la "Bridge"onyesha "Request a bridge from torproject.org" kisha bofya "Request a Bridge..." ili BridgeDB ikupatie bridge. Kamilisha Captcha kisha na bofya "Submit". Bofya "Connect"kuweka mipangilio yako.
Au, kama Tor Browser inatumika, bofya "Settings" katika machaguo (≡)na kisha katika "Connection" katika mstari wa pembeni. Katika sehemu ya "Bridges", tafuta "Request a bridge from torproject.org" and click on "Request a Bridge..."ili ridgeDB ikupatie bridge. Kamilisha Captcha kisha na bofya "Submit". Mpangilio wako kiautomatiki utahifadhiwa mara utapofunga tabo.
Kama unaanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza, bofya katika "sanidi muungamisho"kufungua ukurasa wa mpangilio wa Tor. Chini ya eneo la "Bridge", kutoka katika machaguo "Ingiza anwani ya bridge ambayo unaijua tayari" bofya katika Bridge" na ingiza kila anwani ya bridge katika mstari tofauti. Bofya "Connect"kuweka mipangilio yako.
Au, kama Tor Browser inatumika, bofya "Settings" katika machaguo (≡)na kisha katika "Connection" katika mstari wa pembeni. Chini ya eneo la "Bridge", kutoka katika machaguo "Ingiza anwani ya bridge ambayo unaijua tayari" bofya katika Bridge" na ingiza kila anwani ya bridge katika mstari tofauti. Mpangilio wako kiautomatiki utahifadhiwa mara utapofunga tabo.
Kama mawasiliano hayatafanikiwa, daraja ulilopokea linaweza kuwa na kasi ndogo. Tafadhali tumia moja kati ya njia hapo juu kupata anwani za bridge nyingi zaidi, na jaribu tena.
Kila anwani ya bridge inawakilishwa na mfuatano wa herufi na tarakimu zinazoitwa Bridge-mojis. Bridge-mojis zinaweza kutumika kuhakiki kuwa bridge iliyokusudiwa imewekwa kwa usahihi.
Bridge-mojis ni vitambulisho vya bridge vinavyoweza kusomeka na binadamu na hufanyasiyohuwakilisha ubora wa mawasiliano katika mtandao wa Tor au hali ya bridge. Mfululizo wa alama haziwezi kutumika kama mahitaji. Watumiaji wanahitaji kutoa anwani ya bridge iliyokamilika ili waweze kuunganishwa na bridge.
Anwani ya bridge inaweza kusambazwa kwa kutumia QR code au kwa kuandika anwani husika.
Kanuni ya QR
Unapounganishwa katika tovuti, sio tu waendeshaji wa tovuti husika wanakuwa na uwezo wa kuchukua taarifa zako kuhusiana na ulivyotembelea. Tovuti nyingi sasa hutumia huduma toka kwa watoa huduma wa nje mbalimbali, ikijumuisha mitandao ya kijamii "kama"vitufe, wadukuzi wa uchambuzi na nguzo za matangazo zote ambazo huunganisha shughuli zako toka tovuti mbalimbali.
Kutumia Tor mtandao huzuia wafuatiliaji kutambua eneo ulilopo na anwani yako ya IP, lakini bila hata ya hii taarifa wanauwezo wa kuunganisha maeneo tofauti ya shughuli zako pamoja. Kwa sababu hii, Tor Browser hujumuisha baadhi ya tabia za ziada ambazo zinakusaidia kudhibiti aina ya taarifa za kuwa katika utambulisho wako.
Tor Browser hukusanya uzoefu wako katika mtandao kuhusiana na mahusiano yako na tovuti katika sehemu ya URL. Hata kama utaunganisha katika tovuti mbili tofauti ambayo zinatumia watoa huduma wa nje wanaofanana katika shughulki za ufuatiliaji, Tor Browser italazimisha maudhui kuifadhiwa katika Tor Circuit mbili tofauti ili mfuatiliaji asijue kuwa mawasiliano yote yalitokea katika kivinjali chako.
Kwa upande mwingine, mawasiliano yote katika anwani moja ya tovuti yatakuwa yakifanywa katika Tor Circuit ileile, kumaanisha kuwa unaweza kuperuzi katika kurasa tofauti za tovuti moja katika window tofauti, bila kupoteza namna yoyote ya utendaji kazi.
Unaweza kuona mchoro wa circuit ambao Tor Browser inatumia katika kurasa iliyowazi katika menyu tovuti ya taarifa, katika sehemu ya URL.
Katika circuit,Guard au entry node ni node ya kwanza na huchaguliwa mojakwamoja bila mpangilio maalum na Tor. Lakini ni tofauti na nodes nyingine katika circuit. Ili kuepuka kuhakiki shambulio, Guard node hubadilika baada ya miezi 2-3, tofauti na nodes nyingine,ambayo hubadilika na kila kikoa kipya. kwa taarifa zaidi kuhusiana na Guards, fuatilia FAQ na Support Portal.
Japokuwa Tor Browser imetengenezwa ili kuzuia kufahamika kabisa kwa mtumiaji katika tovuti, kunaweza kuwa na hali ambayo inamfanya mtumiaji kutumia Tor na tovuti ambazo zinahitaji jina la mmtumiaji, nenosiri au taarifa zingine za utambuzi.
Kama utaingia katika tovuti kwa kutumia kivinjari cha kawaida, pia utaonesha anwani yako ya IP na eneo ulilopo katika mchakato huo. Pia hii hutokea unapotuma barua pepe. Unapoingia katika mitandao yako ya kijamii au akaunti za barua pepe kwa kutumia Tor Browser inakuruhusu kuchagua aina gani ya taarifa za kuweka wazikatika tovuti unayoperuzi. Kuingia kwa kutumia Tor Browser pia inafaa kama tovuti unayoingia ipo salama katika mtandao wako.
Kama utaingia katika tovuti kwa kutumia Tor, kuna vitu mbalimbali vya kuzingatia:
Machaguo ya sifa za Tor Broswer za “New Identity” na “New Tor Circuit kwa tovuti hii". Pia zinapatikana katika menyu kuu au menyu iliyofichwa (≡).
Machaguo haya yatafaa kama, unataka kuzuia shughuli za baadae za kivinjari kuunganishwa na kile ulichokuwa unafanya kabla. Kuichagua hii itafunga kurasa zote zilizo wazi, kufuta taarifa zote binafsi kama vile vidakuzi na historia ya kuperuzi, na kutumia Circuit mpya ya Tor kwa mawasiliano yote. Tor Brpwser itakuonya kuwa shughuli zoten na kupakua zitasitishwa, kwahiyo zingatia hili kabla huja bofya “New Identity”.
Kutumia chaguo hili, utahitajika kubofya'New Identity' katika mstari wa machaguo wa Tor Browser's toolbar.
Chaguo linaweza kutumika kama exit relay unayotumia haina uwezo wa kuunganisha katika tovuti unayohitaji, au haifungui vizuri. Kuichagua kutasababisha kurasa iliyo wazi kufunguliwa katika Tor Circuit mpya. Kurasa zingine zilizo wazi kutoka katika tovuti moja zitatumia circuit mpya pia pale zitakapo funguliwa tena. Machaguo haya hayatafuta taarifa zozote binafsi au kukata mawasiliano ya shughuli zako katika tovuti.
Pia unaweza pata haya machaguo katika circuit mpya, katika menyu ya taarifa za tovuti, katika sehemu ya URL.
Onion services (formerly known as "hidden services") are services, like websites, that are only accessible through the Tor network.
Onion services hutoa manufaa kadhaa zaidi ya huduma za kawaida za tovuti zisizo binafsi:
Just like any other website, you will need to know the address of an onion service in order to connect to it. An onion address consists of 56 letters and numbers, followed by ".onion".
Unapotumia tovuti inayotumia onion service, Tor Browseritaonyesha katika sehemu ya kuandika URL alama ya onion itaonyesha hali ya mawasiliano yako: salama na kutumia onion service. Unaweza kujifunza zaidi kuhusiana na huduma za onion ambayo unatembelea kwa kuangalia katika sehemu inayoonyesha Circuit.
Njia nyingine ya kujua tovuti ya onion kama msimamizi wa tovuti haiweka tabia ya Onion-Location. Onion-Location ni taarifa ya HTTP isiyo na viwangoambayo tovuti inaweza kutumia kutangaza onion zingine. Kama tovuti unayotembelea ina onion, ujumbe wa zambarau katika sehemu ya URLkatika Tor Browser utatokea ukionyesha "uwepo wa .onion". Ukibofya katika ".onion available",tovuti itatafuta data tena na kukupeleka katika onion zingine.
To always prioritize onion site versions of websites, you can enable automatic Onion-Location redirects.
Click on hamburger menu (≡), go to Settings, click on Privacy & Security, and in the Onion Services section look for the entry "Prioritize .onion sites when known." and check the option "Always".
Or you can copy and paste this URL in a new tab: about:preferences#privacy
and change this setting.
Uthibitisho wa onion service ni huduma ambayo tovuti ya onion ambayo inahitaji mtumiaji atoe namba za uthibitisho kabla ya kupata huduma. As a Tor user, you may authenticate yourself directly in Tor Browser. Ili kupata huduma hii, utahitaji kupata utambulisho toka kwa mto huduma wa onion service. Unapotumia onion service zilizothibitishwa, Tor Browseritaonyesha katika sehemu ya URL alama ndogo ya kijivu, ikiwa na ujumbe wa maelezo. Ingiza alama zako za utambuzi halisi katika sehemu ya kujaza.
Kama huwezi kujiunga katika tovuti ya onion, Tor Browser wataleta ujumbe maalumu wa uwepo wa dosari kutoa taarifa kwanini tovuti haipatikani. Dosari zinaweza kutokea katika matabaka mbalimbali: dosari za mtumiaji, dosari za mtandao au dosari za huduma. Baadhi ya hizi dosari zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kwenda sehemu ya Troubleshooting . Jedwali lifuatalo linaonyesaha dosari zozote zinazoweza kujitokeza na hatua za kuchukua ili kutatua.
Msimbo | Jina la Dosari | maelezo kidogo |
---|---|---|
0xF0 | Tovuti ya onion Haipatikani | Sababu kuu inaweza kuwa tovuti ya onion haipo hewani. Wasiliana na msimamizi wa tovuti ya onion. |
0xF1 | Tovuti ya Onion Haiwezi kupatikana | Tovuti ya onion haipatikani kutokana na dosari za mtandao. |
0xF2 | Tovuti ya onion haijaonganishwa | Sababu kubwa inaweza kuwa tovuti ya onion haiko hewani. Wasiliana na msimamizi wa tovuti ya onion. |
0xF3 | Haiwezi kuunganishwa na tovuti ya onion | Tovuti ya onion inatumika au mtandao wa Tor umezidiwa. Jaribu tena baadaer. |
0xF4 | Tovuti ya onion inahitaji uthibitisho | Ili kuifikia tovuti ya onion kulihitaji alama za utambulkisho na hazikutolewa. |
0xF5 | Uthibitisho wa tovuti ya onion haujafanikiwa | Alama za utambulisho zilizotolewa si sahihi zimekataliwa. Wasiliana na msimamizi wa tovuti ya onion. |
0xF6 | Anwani ya tovuti ya onion sio sahihi | Anwani ya tovuti ya onion sio sahihi. Tafadhali hakikisha umeingiza kwa usahihi. |
0xF7 | Muda wa kutengeneza Circuit ya tovuti ya onion umeisha | Imeshindwa kuunganisha katika tovuti ya onion, inawezekana kutokana na mtandao kuwa dhaifu. |
Kma huwezi kupata onion service ulizoomba, hakikisha umeingiza anwani ya onion kwa usahihi; sababu hata kosa dogo tu itaizuiaa Tor Browser kuipata tovuti hiyo.
If you are trying to access a 16 character (the shorter "V2 format") onion service, this type of address no longer works on today's Tor network.
Unaweza pia kujaribu kama unauwezo wa kupata onion services nyingine bkwa kuunganisha katika DuckDuckGo's Onion Service.
Kama bado unashindwa kujiunga katika onion service baada ya kuthibitisha anwani, tafadhali jaribu tena baadae Kunaweza kuwa na matatizo ya muda katika mtandao, au waendeshaji wa tovuti wanaweza kuiruhusu kutokuwa hewani bila kutoa tahadhali.
Kama taarifa binafsi kama kuingiza nenosiri zikisafirishwa bila kusimbwa katika mtandao, iinaweza kiutambuliwa kwa urahisi na watu wasiohusika. Kama unaingia katika tovuti yoyote, yhakikisha kwamba tovuti ina usimbwaji wa HTTPS , ambao hulindwa na wadukuzi wa aina hii.Unaweza kuhakiki hii katika sehemu ya URL: kama mawasiliano yako yamesimbwa, anwani itaanza na “https://”, badala ya“http://”.
Mfumo pekee wa HTTPS-hulazimisha mawasiliano yote katika tovuti kuwa salama na kuwa yaloiyosimbwa huitwa HTTPS. Tovuti nyingi sasa hutumia HTTPS; baadhi hutumia zote HTTP na HTTPS. Kuruhusu mfumo huu katika mawasiliano yako ya tovuti yatawezeshwa kutumia HTTPS na yatakuwa salama.
Baadhi ya tovuti hukubali HTTP pekee na mawasiliano hayawezi kuboreshwa. Kamatoleo la HTTPS ya tovuti inapatikana, utaona kurasa ya “mawasiliano salama hayapo”:
Kama utabofya 'endelea katika tovuti ya HTTP ' umekubali hatari na utatembeleatovuti ya toleo la HTTP. Mfumo wa HTTPS-Only utazimwa kwa muda katika tovuti.
Bofya kitufe cha 'Go Back' kama unataka kukwepa mawasiliano yasiyo simbwa.
Mchoro ufuatao unaonyesha taarifa zipi zinaonekana kwa wasikilizaji wa siri ukitumia au usipotumia usimbwaji wa Tor Browser na HTTPS:
Mojakwamoja, Tor Browser hulinda usalama wako kwa kusimba data unazo peruzi. Unaweza kuchagua kuongeza usalama zaidi kwa kuchagua kuondoa baadhi ya tabia za tovuti ambazo zinaweza kutumika kusumbua usalama wako na kutojulikana. Unaweza kufanya hii kwa kuongeza kiwango cha usalama Tor Browser katika menyu. Kuongeza kiwango cha ulinzi katika Tor Browses kutazuia baadhi ya tovuti kufanya kazi vizuri, shivyo unatakiwa upime mahitaji ya ulinzi wako kutokana na matumizi na mahitaji yako.
Usalama wa kimpangilio unaweza kupatikana kwa kubonyeza Ngao ikon ijayo kwenye Tor Kivinjari URL baa. To view and adjust your Security Settings, click on 'Settings' button in the shield menu.
Kuongeza kiwango cha ulinzi katika Tor Browser mpangilio wa ulinzi utazuia au utazuia baadhi ya tabia kulinda na uvamizi unaoweza kutokjea. Unaweza kuwezesha mipangilio hii tena katika muda wowote kwa kurekebisha kiwango cha Usalama wako.
Kiwango hiki kinazuia tabia za tovuti ambazo ni hatari. Hii inaweza kusababisha baadhi ya tovuti kushindwa kufanya kazi.
JavaScript haijawezeshwa katika tovuti zote zisizo naHTTPS ; baadhi aina ya maneno na alama za hesabu hazijawezeshwa; sauti na video (HTML5 ni bofya ili kucheza.
TKiwango hiki huruhusu tabia za tovuti zinazohitajika katika tovuti za kuduma na huiduma za msingi. Mabadiliko haya huathili picha, nyimbo na video na maandishi.
Javascript imezuiliwa mojakwamoja katika kila tovuti; baadhi ya aina ya maneno, nembo, alama za hesabus, na picha hazijawezeshwa; sauti na video (HTML5 media)bofya ili kucheza.
Tor Browser ni lazima isasishwe wakati wote. Kama unaendelea kutumia toleo lililopitwa na wakati la programu, unaweza kuwa katika hatari ya kupata tatizo kubwa la kiusalama ambazo zitasumbua faragha na kutojulikana kwako.
Tor Browser itakusisitiza kusasisha programu pale tu toleo jipya litakapo toka:menyu kuu (≡)itaonyesha duara la kijani ikiwa na mshale ulioangalia juu, na unaweza kuona kiashiria cha kusasisha kila ukifungua Tor Browser. Unaweza kusasisha mojakwamoja katika mfumo au wewe mwenyewe.
When you are prompted to update Tor Browser, click on the main menu (≡), then select "Update available - restart now".
Subiria maboresho kisha pakua na sakinisha, kisha Tor Browser itaanza yenyewe. Sasa utakuwa unatumia toleo jipya.
Unaposisitizwa kusasisha Tor Browser, maliza shughuli ya kuperuzi kisha funga programu.
Ondoa Tor Browser katika mfumo wako kwa kulifuta folda lililomo (angalia sehemu ya kuondoa usanikishajifokwa taarifa zaidi).
Tembelea https://www.torproject.org/download/ na upakue nakala ya toleo jipya la Tor Browser lililotolewa, kisha sakinisha kama mwanzo.
Unatakiwa kuanza kuperuzi tovuti kwa kutumia Tor Browser smuda mfupi baada ya kutumia programu, na bofya kitufe cha “Connect” kama unatumia kwa mara ya kwanza.
Connection Assist hukutaarifu juu ya hali ya uunganishwaji katika mtandao wako kama uta bofya katika 'Test'.
Check your Internet Connection if it says 'Offline'. If your connection to the Tor Network is not established and it reads 'Not Connected' the following steps can be helpful.
Kama Tor Browser haiunganishwi, kunaweza kuwa na sukuhusho rahisi. Jaribu kila kimoja katika vifuatavyo:
Mara nyingi, ili kuangalia matatizo ya Torinaweza kusaidia katika kuchunguza tatizo. Kama unapata changamoto katika kuunganisha, ujumbe wa dosari unaweza kutokea na unaweza kiuchagua "copy Tor log to clipboard". Kisha nakili matatizo ya Tor log katika faili la kipimo au nyaraka nyingine.
Kama huoni chaguo hilo na Tor Browser imefunguliwa,Unaweza kutafuta katika menyu iliyofichwa ("≡"),kisha bofya katika "Settings", na mwishoni katika "Connection" sehemu ya machaguor. Chini katika kurasa, pembeni ya maandishi ya "View the Tor logs", bofya kitufe cha "View Logs...".
Njia mbadala, katika GNU/Linux, kuona tatizo hapohapo katika kifaa, peruzi katika saraka ya Tor Browserna ianzishe kutumia Tor Browser kutoka katika sehemu ya amri:
./start-tor-browser.desktop --verbose
Ili kuhifadhi tatizo katika faili (default: tor-browser.log):
./start-tor-browser.desktop --log [file]
Taarifa zaidi kuhusiana na hii zinaweza kupatikana katika Support Portal.
Kama bado huwezi kuunganisha na,Mtoa huduma wako wa mtandao anaweza kuwa amezibiti mawasiliano katika Tor network. Soma sehemu yaKukwepa udhibiti kwa ajili ya masuluhisho yanayowezekana.
Tor Browser inaendelea kuboreshwa, na kuna baadhi ya matatizo yanajulikana lakini bado hayaja tatuliwa. Tafadhalki angalia kurasa ya Matatizo yanayojulikana kuona kama tatizo unalopitia limeorodheshwa.
JavaScript ni lugha ya programu ambayo tovuti hutumia kutoa vitu vya kimawasiliano kama vile, video fupi, sauti, na thali katika muda. Bahati mbaya, JavaScript pia inaweza kuruhusu kuvamiwa katika ulinzi wa kivinjari, ambayo hupelekea hali isiyo ya kawaida.
Tor Browser inavitu vya ziada viitwavyo NoScript. Hupatikana kupitia "Preferences" (au"Options" katika Windows) ya hamburger menu (≡), kisha chagua 'Customize' kisha vuta alama ya “S” iliyopo juu kulia katika window. NoScript inakuruhusu kudhibiti JavaScript (na aina zingine za scripts) zilizopo katika tovuti binafsi, au bhuzuia kabisa.
Watumiaji wanahitaji kiwango kikubwa cha ulinzi katika kuperuzi katika mitandao wanatakiwa kuweka Tor Browser’s Kiwango cha ulinzi)katika Safer” (ambayo huzuia JavaScript katika tovuti zisizo na HTTPS ) au “Safest” (ambazo hufanya hivyo kwa tovuti zote). Hatahivyo, kuizuia JavaScript itazuia tovuti nyingi kuonyehs kwa usahihi, hivyo mpangilio wa mojakwamoja wa Tor Browser ni kuruhusu tovuti kutumia scripts katika mfumo wa "Standard".
Tor Browserinapatikana katika Firefox, na inaweza kuongezwa katika kivinjari kingine chochote au maudhui yanayoendana na Firefox yanaweza kusakiniwa katika Tor Browser.
Hatahivyo, vitu pekee vilivyoongezwa ambavyo vimejaribiwa kwa matumizi na Tor Browser ni vile vilivyojumuishwa mojakwamoja. kusanikisha kivinjari kingine chochote inaweza kuzuia utendaji kazi wa in Tor Browser au kusababisha matatizo makubwa zaidi ambayo yanaathili usalama na faragha yako. Haishauriwi kabisa kuongeza vitu vingine, na Tor Project haitatoa msaada kwa usanidi huo.
Flash was a multimedia software used by websites to display video and other interactive elements such as games. It was disabled by default in Tor Browser because it could have revealed your real location and IP address. Tor Browser no longer supports Flash and cannot be enabled.
The majority of Flash's functionalities have been substituted by the HTML5 standard, which heavily depends on JavaScript. Video platforms such as YouTube and Vimeo have transitioned to HTML5 and no longer utilize Flash.
Kutoa Tor Browserkatika mfumo wako ni rahisi:
Kwenye Windows:
Kwenye macOS:
~/Library/Application Support/
.~/Library/Application Support/
katika windo kisha bofya Go.Zingatia kama hujasakini Tor Browser katika sehemu yake halisi (folda la program), kisha folda la data za TorBrowser fhaijawekwa katika ~/Library/msaada wa programu/
folda, lakini katika folda hilohilor ambalo umesakini Tor Browser.
Katika Linux:
Zingatia viwango vya utendaji wa mashine yako upande wa "Uninstall" haitumiki.
Tor huitaji muda wa mfumo wako (na majira ya kanda yako) kuwekwa katika muda sahihi.
Program za kuzuia virusi na program hatarishi humzuia mtumiaji kupata Tor Browser. Wakati mwingine huleta ujumbe wa false positives regarding malware and/or vulnerabilities. Unaweza kusoma zaidi kuhusiana na hii katika Support Portal. Programu zifuatazo za kuzuia virusi zimefahamika kuingilia Tor na zitatakiwa kutowezeshwa kufanya kazi kwa muda mfupi:
Pia VPN huwa na tabia ya kuingilia Tor na huitajika kuzimishwa. Pia tunashauri kuto tumia VPN pamoja na Tor labda uwe mtumiaji mzoefu ambaye anajua namna ya kuziweka sawa ili zikubaliane na faragha yako. Unaweza kupata taarifa zaidi za Tor+VPN katika awani yetu wiki.
Video zinazohitaji flash ya Adobe hazipo. Flashi haiwezi kufanya kazi kwa ajili ya sababu za kiusalama.
Tor haiwezi kutumia bridge kama kifaa cha kati ya mawasiliano kitatumika.
Programu ya Tor Browser imepewa tarehe ya Januari 1, 2000 00:00:00 UTC. Hii ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kila programu iliyotengenezwa inauwezo sahihi.
Namna ya kuifanya Tor Browser kama kivinjari chako cha kutumia wakati wote default browser.
Kama Tor Browser ilikuwa inafanya kazi kabla na haifanyi kazi sasa (hususani baada ya kusanikisha tena aukuhuwisha), mfumo wako unaweza kuwa umelala . Kuzima na kuwasha upya mfumo wako. kwa jambo hilo, litatatua tatizo.
Tor haitaanza kufanya kazi wakati njia ya folda ina alama zisizo na mfumo wa ASCII.
Utaratibu wa kuhamisha mafile makubwa siyo isiyotambulika kwa Tor.
Tor Browser ya Android ni programu pekee iliyo rasmi kwa ajili ya vifaa vya mkononi inayowezeshwa na kutengenezwa na Tor Project. Ni kama Tor Browser ya kompyuta, lakini ni kwa vifaa vya android vya mkononi. Baadhi ya sifa za kipekee za Tor Browser ya Android inahusisha :kupunguza kufuatilia tovuti, kutambua ufuatiliwaji, kukabili utambuzi wa kipekee wa kivinjari, na kukwepa udhibiti.
Hapo inakaa Tor Browser ya android na Tor Browser ya Android (alpha). Watumiaji wasio wataalamu wanatakiwa kupata Tor Browser ya android, sababu hii inautulivu na ina dosari chache sana. Tor Browse ya Android inapatikana katika Play Store, F-Droid na tovuti ya Tor Project. Ni hatari sana kupakua Tor Browser nje ya sehemu hizi tatu.
Unaweza kusakinisha Tor Browser ya Android kutoka katika Google Play Store.
The Guardian Project hutoa Tor Browser ya Android katika hifadhi zao za F-Droid. Kama utapenda kusakinisha programu kutoka katika F-Droid, tafadhali fuata hatua zifuatazo:
Sakinisha program ya F-Droid app katika kifaa chako cha Android kutoka the F-Droid website.
Baada ya kusakinisha F-Droid, fungua programu.
3.Kona ya kulia chini, Fungua "Settings".
Chunu ya sehemu ya "My Apps", fungua sehemu ya kuhifadhi data.
Geuza"Guardian Project Official Releases" kama iliyo wezeshwa.
Sasa F-Droid hupakua orodha ya programu kutoka katika hazina ya Guardian Project(Zingatia: hii inaweza chukua dakika kadhaa).
Bofya kitufe cha kurudi katika kona ya kushoto juu.
Fungua"Latest" katika kona ya kushoto chini.
Fungua ukurasa wa kutafuta kwa kubofya sehemu ya kukuza uoande wa kulia chini.
Tafuta "Tor Browser ya Android".
Fungua taarifa za matokeo kwa "Tor Project" kisha sakinisha.
Pia unaweza kuipatat Tor Browser ya Android kwa kupakua na kusakinisha apk kutoka katika Tor Project website.
Unapotumia Tor Browser kwa mara ya kwanza, yutapata machaguo ya kuunganisha mojakwamoja katika mtandao wa Tor, au kusanidi Tor Browser kwa ajili ya mawasiliano yako katika alama ya mpangilio.
Mara nyingi, kuchagua"Connect" itakuruhusu kuunganisha katika mtandao wa Tor bila usanidi wa ziada. Pale tu inapoguswa. kutatokea kubadilishwa kwa sentensi chini ya skrini, ikionesha kuendelea kwa mawasiliano ya Tor. Kama upo katika mawasiliano yenye kasi ya haraka, lakini ujumbe huu unaonekana kukwama mahali, angalia kurasa ya Troubleshooting kupata msaada wa kutatua tatizo hilo.
Kama unajua kuwa mawasiliano yako yamedhibitiwa, unatakiwa kuchagua kitufe cha mpangilio. Tor Browser itakupeleka katika machaguo kadhaa ya kusanidi. Skrini ya kwanza itakupa taarifa ya hali ya mtandao wa Tor na kukupa chaguo la kusanidi Bridge ('Config Bridge'). Kama unajua mtandao wako umedhibitiwa au umejaribu na umeshindwa kujiunga katika mtandao wa Tor na hakuna suluhisho lingine limepatikana, bofya katika 'Config Bridge'. Utapelekwa katika Kukwepa udhibiti kurasa ya kusanidi pluggable transport.
Relays za Bridge ni relays za Tor ambazo hazitaorodheshwa katika umma ya sakara ya Tor. Bridges hufaa kwa watumiaji wa Tor bila sheria, na kwa watu wanaohitaji tabaka za ziada la ulinzi sababu wanahofia mtu anaweza kuwatambua kuwa wanawasiliana kutumia anwani ya IP ya Tor relay.
Kutumia pluggable transport, bofya katika alama ya mpangilio unapoanza Tor Browser kwa mara ya kwanza. Skrini ya kwanza inaelezea hali ya mtandao wae Tor. Bofya katika'Config Bridge' ili kusanidi bridge.
Skrini inayofuata itakupa chaguo la kutumia bridge iliyoundwa katika mfumo au bridge ya kutengeneza. Kwa kutumia chaguo la "Use a Bridge"utakuwa na machaguo matatu: "obfs4", "meek-azure", and "snowflake".
Kama utachagua chaguo la "Provide a nBridge I know",kisha utahitajika kuweka bridge address.
Wakati Tor Browserinafanya kazi, utapata taarifa katika kifaa chako baada ya kufungua taarifa ya "NEW IDENTITY". Kubofya katika kitufe hicho kitakulketea new identity. Kinyume na Tor Browser ya kompyuta, kitufe cha "NEW IDENTITY"katika Tor Browser ya Android haizuii shughuli za kivinjali chako kinachofuata kuunganishwa na kile ulichokuwa unafanya kabla. Kwa kuchahua hivyo itabadilisha Tor circuit yako.
Mpangilio wa ulinziondoa baadhi ya tabia za tovuti ambazo zinaweza kusumbua ulinzi na kutofahamika. Tor Browser ya Android hutoa hatua zilezile tatu za ulinzi ambazo zinapatikana katika kompyuta. Unaweza kuboresha kiwango cha usalama kwa kufauata hatua zifuatazo:
Tor Browser ni lazima isasishwe wakati wote. Kama unaendelea kutumia toleo lililopitwa na wakati la programu, unaweza kuwa katika hatari ya kupata tatizo kubwa la kiusalama ambazo zitasumbua faragha na kutojulikana kwako. Unaweza kusasisha Tor Kivinjari kiautomatiki au kiumongozo.
Njia hii huamini kwamba inaweza ukawa na Google Play or F-Droid imesanidiwa katika kifaa chako cha mkononi.
Bofya katika "Settings", kisha nenda katika "Manage installed apps". Katika skrini inayofuata, chagua Tor Browser kisha bofya kitufe cha "Update".
Tembelea tovuti ya Tor Project pakua nakala ya toleo jipya la Tor Browser, kishasakinisha kama ilivyokuwa mwanzo. Mara nyingi, toleo hili jipya la Tor Browser hujisanikisha katika toleo la zamani, hivyo huboresha kivinjari. Kama kufanya hivi itashindwa kusasisha kivinjari, unaweza kuhitajika kuitoa Tor Browserkabla ya kusakinisha. Tor Browser ikiwa imefungwa, toa katika mfumo wako kwa kutumia mpangilio wa programu ya kifaa chako. Kulingana na aina ya kifaa chako, nenda katika Settings > Apps, kisha chagua Tor Browser kisha bofya kitufe cha "Uninstall" . Baada ya hapo, pakua toleo jipya la Tor Browser kisha sakinisha.
Tor Browser ya Android inaweza kutolewa mojakwamoja kutoka katika F-Droid, Google Play au kutoka katika mpangilio wa programu wa kifaa chako cha mkononi.
Bofya katika "Settings", kisha nenda katika "Manage installed apps". Katika skrini ifuatayo, chagua Tor Browser na kisha bofya katika kitufe cha "{uninstall".
Kulingana na aina ya kifaa chako, Nenda katika mpangilio > Apps, kisha chagua Tor Browser bofya katika klitufe cha "Uninstall".
Kungalia dosari katika Tor yako:
If you want to share the error logs with us, you can take a screenshot. By default, screenshots are disabled in Tor Browser, but you can enable them. To do this, please follow these steps:
Kusuluhisha baadhi ya matatizo ya kawaida tafadhali zingatia katikaSupport Portal entry.
Wakati mwingine, kuna baadhi ya vitu havipo katika Tor Browser ya Android, lakini kwa kawaida vipo katika Tor Browser ya kompyuta.
Orfox kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2015 na mradi wa The Guardian, kwa lengo la kuwapatia watumiaji wa android njia ya kuperuzi mtandaoni kwa kutumia Tor. Kwa maiaka mitatu iliyofuata ,Orfox iliboreshwa na kuwa namna maarufu ya watu kuperuzi kwa faragha zaidi kuliko kivinjari kingine vya kawaida, na Orfox ikawa muhimu katika kusaidia watu kukwepa udhibiti wa mtandao na kuzipata tovuti zilizozuiliwa na vyanzo muhimu. Mwaka 2019, Orfox iliisha baada ya Tor Browser rasmi ya Android kuanzishwa.
Orbot ni programu huru ya proxy ambayo inawezesha programu zingine kutumia mtandao wa Tor. Orbot hutumia Tor kusimba usafirishaji wa data zako mtandaoni. Kisha unaweza kutumia pamoja na programu zingine zilizosanidiwa katika kifaa chako cha mkononi ili kukwepa udhibiti na kulinda ufuatiliwaji. Orbot inaweza kupakuliwa na kusakinishwa kutoka katika Google Play. Angalia our Support portal kama unahitaji vyote Tor Browser ya Android naOrbot kimoja wapo.
Hakuna Tor Kivinjari kwa iOS. Tunashauri proramu ya iOS inayoitwa Onion Browser, ambayo inapatikana bure kwa uwazi, kutumika kusafirisha, na imetengenezwa na mtu ambaye anafanya kazi kwa ukaribu na Tor Project. Hatahivyo, Apple huitaji kivinjari katika iOS kutumia kitu kinaitwa Webkit, ambayo huzuia Onion Browser kuwa na ulinzi wa faragha kama uliopo katika Tor Browser.
Jifunze zaidi kuhusu Onion Kivinjari. Pakua Onion Kivinjari kwenye App Store.
Kwa sasa hakuna njia inayokuwezesha kutumia Tor katika simu window za zamani lakini kwa simu za toleo jipya zenye mfumo mpya wa microsoft fuata hatua kupitia Tor Browser on Android zinaweza kufauatwa.
Kama unapendelea, Tor Kivinjari inaweza kufanya kubeba kwa kuiondoa kwenye kumbukumbu yake moja kwa moja kwenye media inayoweza kutolewa kama vile fimbo ya USB au kadi ya SD. Inashauriwa kutumia kifaa kinachoandikika ili Tor Browser iweze kusasisha kama inavyotakiwa.
Kwa Windows:
Weka katika kifaa chako kinachoweza kutolewa kisha unda upya. Mfumo wowote wa faili utafanya kazi.
Peruzi katika Tor Browser pakua kurasa.
Pakua faili la Windows .exe
kisha hifadhi katika kifaa chako.
(Imeshauriwa) Hakiki saini za mafaili.
Upakuaji ukikamilika, bofya faili la .exe
na anza kusanikisha.
Ikihitaji kujua sehemu ya kusanikisha Tor Browser, chagua kifaa chako kinachoweza kuwekwa na kutolewa.
Kwa macOS:
Chomeka katika kifaa chako kinachoweza kutolewa. Ni lazimautumie Mac OS Extended iliyo katika mfumo (ulioandika).
Peruzi katika Tor Browser pakua kurasa.
Pakua faili la macOS .dmg
kisha hifadhi katika kifaa chako.
(Imeshauriwa) Hakiki saini za mafaili.
Upakuaji ukikamilika, bofya faili la .dmg
na anza kusanikisha.
Ikihitaji kujua sehemu ya kusanikisha Tor Browser, chagua kifaa chako kinachoweza kuwekwa na kutolewa.
Kwa GNU/Linux:
Weka katika kifaa chako kinachoweza kutolewa kisha unda upya. Mfumo wowote wa faili utafanya kazi.
Peruzi katika Tor Browser pakua kurasa.
Pakua faili la wazi.tar.xz
na hifadhi katika kifaa chako.
(Imeshauriwa) Hakiki saini za mafaili.
Upakuaji ukikamilika, rudisha mafaili halisi katika kifaa chako pia.
Unapotuma maombi ya kupata msaada,Mrejesho au kutoa taarifa ya tatizo, tafadhali jumuisha taarifa nyingi kadri uwezavyo:
Kuna njia mbalimbali za kuwasiliana nasi,tafadhali chagua ipi itakufaa zaidi.
Tuna Telegram bots na njia za mawasiliano rasmi:
Tunashauri kuomba msaada katika Jukwaa laTor. Ili kuwasilisha mada mpya itakubidi utengeneze akaunti. Tafadhali pitia majadiliano yetu ya miongozo kisha angalia mada zilizopo kiabla ya kuuliza. Kwasasa, kwa majibu ya mwisho, tafadhali andika kwa kingereza. Kama utapata tatizo, tafadhali tumia GitLab.
Unaweza kuwasiliana na nasi kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya WhatsApp: +447421000612. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa.
Unaweza kupata msaada kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya Signal: +17787431312. Signalni programu ya matumizi ya bure na imelenga ufaaragha kwa watumiaji. kwasasa, mfumo wetu wa msaada unapatikana kwa lugha ya kingereza na kiurusi katika kusaidia watumiaji wa Tor kwa maeneo yaliyodhibitiwa. Huduma hii hupatikana kwa ujumbe mfupi wa maneno tu; video, au simu hazijawezeshwa. Baada ya kutuma ujumbe,watu wetu wa msaada watakusaidia kutatua tatizo.
Tutumie barua pepe kupitia frontdesk@torproject.org
Katika kichwa cha habari cha barua pepe yako, tafadhali tujulishe unatoa taarifa ya kitu gani. Namna ambavyo kichwa cha habari cha barua pepe kinakuwa mahususi mfano. "Kushindwa kuunganishwa", "mrejesho katika tovuti", "Mrejesho katika Tor Browser, "Nahitaji bridge"), ndivyo itakavyokuwa rahisi kwetu kuelewa na kufuatilia. Wakati mwingine tunapopokea barua pepe zisizo na kichwa cha habari,huingia katika barua pepe zisizothibitishwa na tunashindwa kuziona.
Kwa mrejesho wa mwisho, tafadhali andika katika lugha za kingereza, kiurusi, kihispaniola, kihindi kibangaladeshi//au kireno kama unaweza. Kama hakuna lugha unayoielewa kati ya hizi, tafadhali andika kwa lugha yoyote unayoweza, lakini jua kwamba muda kidogo kujibu sababu tutahitaji msaada wa kutafsiriwa ili kuelewa.
Unaweza kutupata katika #tor
njia ya OFTC au chaneli ya kutoa msaada kwa watumiaji wa Tor katika Matrix. Tunaweza tusijibu papo kwa hapo, lakini tunaangalia matatizo yaliyopita na tutakurudia tunapoweza.
Jifunze namna ya kujiunganisha katika IRC / Matrix.
Kwanza, angalia kama tatizo limejulikana. Unaweza kutafuta na kusoma matatizo katika https://gitlab.torproject.org/. Kuunda jambo jipya, tafadhaliomba akaunti mpya kuipata Tor Project's GitLab haraka na tafuta hifadhi sahihi kutoa taarifa ya tatizo. Tunafuatilia matatizo yote yahusianayo na Tor Browser Tor Browser issue tracker. Matatizo yahusianayo na tovuti yetu yanatakiwa kujazwa katika Kinasa matatizo ya tovuti.